1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Haiti wakubaliana kuunda serikali ya mpito

9 Aprili 2024

Viongozi wa Haiti wamekamilisha makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya muda ili kuliondoa taifa hilo la Karibian katika machafuko yanayochochewa na magenge.

https://p.dw.com/p/4eZqG
Jamaika CARICOM
Jumuiya ya Mataifa ya Karibian (CARICOM) wakijadili hali halisi ya HaitiPicha: Andrew Caballero-Reynolds via REUTERS

Makubaliano hayo yanajumuisha baraza la wanachama tisa, lenye wapiga kura saba na waangalizi wawili, wanaowakilisha vyama vya siasa, sekta ya kibinafsi na mashirika ya kiraia, ambayo yatafungua njia kwa uchaguzi wa rais mapema 2026.

Jukumu la kwanza la baraza hilo ni kumchagua waziri mkuu ambaye, kwa ushirikiano na baraza hilo ataunda serikali yenye dhamana ya kuongoza nchi hadi "uchaguzi wa kidemokrasia, huru na wa kuaminika" utakapofanyika.

Zaidi ya watu 50,000 wakimbia mji mkuu wa Haiti

Aidha wajumbe wa baraza hilo au serikali itakayoundwa hivi karibuni hawatoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.

Kulingana na makubaliano hayo yaliyowasilishwa kwa Jumuiya ya Mataifa ya Karibia (CARICOM)mamlaka ya baraza hilo yatakamilika mnamo Februari 7, 2026.

Hata hivyo maelezo ya makubaliano hayo lazima yaidhinishwe na mamlaka inayoondoka madarakani.